Friday, October 4, 2013

SHAKEEL INVESTMET : SUPRISE ALIYOFANYIWA NA KIPENZI CHAKE PENNIEL


HABARI ZAIDI habani26.blogspot.com/2013/10/suprise-aliyofanyiwa-na-kipenzi-chake.html

SUPRISE ALIYOFANYIWA NA KIPENZI CHAKE PENNIEL


 
 Kila mtu anaithamini na kuipenda tarehe ya siku 
yake ya kuzaliwa,ni siku ambayo baadhi yetu huifurahia kwa
 mitindo tofauti tofauti kulingamna 

na nafasi aliyonayo mtu husika,lakini hebu
 jiulize how it feels ndani ya hiyo siku mhimu kabisa 
unapofanyiwa kitu kizuri na cha pekee na mtu
 mhimu maishani mwako,inapendeza siyo?hivyo ndivyo
 nilivyojiskia siku ya jana baada ya 
kufanyiwa suprise ya  birthday party
 na kipenzi changu,Penniel pamoja
 na Mama yangu mpenzi,dada yangu Esma,Halima kimwana 
na familia yangu kwa ujumla.
checkout picha zikijieleze zenyewe........
 
 
Ilikuwa ni baada ya kutoka kwenye
uzinduzi wa Coke studio,kufika nyumbani
Nikapokelewa kwa bashasha na Dada angu Queen Darlin(aliyeshikilia cake) 
 
 
Dada angu Esma na mmoja wa rafiki wa familia yangu pamoja na Shilole nae alikuwep kusapoti 
 
Baby akanisuprise kwa Kiss mwanana kabisa , like duuuh!!! 
 
Nyakati kaama hizi mamabo ya maakuri kama hivi huwa hayakosekani
  
Kupendwa ndio huku..Mtoto wa bi Sandra mie
  
 

KAMA ULIMISI HIZI NDIO PICHA ZA SIKU YA BIRTHDAY YA DIAMOND



 















Wednesday, September 25, 2013

YANGA YAJIANDAA KUIKABILI RUVU SHOOTING


KIKOSI CHA YANGA

Young Africans imeendelea na mazoezi leo katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola-Mabibo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumaosi dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa jumamosi ni muhimu kwa timu ya Young Africans kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake na kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya timu inayoongoza kwa tofauti ya pointi 5.

Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts ameendelea kuyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita kwa lengo la kuhakikisha vijana wake wanakua makini na kuzitumia vizuri nafasi wanazozipata.

Ikiwa imecheza mitano ikishinda mchezo mmoja, sare michezo mitatu na kufungwa mchezo mmoja, Young Africans imefanikiwa kukusanya pointii 6 na kufunga mabao 10 na kufungwa mabao 7.

Kikosi kinatarajiwa kuingia kambini kesho katika hosteli za klabu kujiandaa na mchezo huo wa jumamosi dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting.